Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA-USALAMA

Hali nchini Libya: Maafisa wa Urusi na Uturuki wakutana

Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Cavusoglu alisema Jumatano kwamba nchi yake na Urusi zinakaribia makubaliano juu ya Libya baada ya siku mbili za mazungumzo mapya huko Ankara.

Vikosi vya Jeshi la taifa la Libya huko Bengazhi.
Vikosi vya Jeshi la taifa la Libya huko Bengazhi. Abdullah DOMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yaligubikwa hasa na kudumisha mkataba wa usitishwaji wa mapigano na kurudi kwa mchakato wa kisiasa.

Vita vya Libya ni vita vya washirika. Nchi nyingi za kigeni zinahusika katika suala hili. Uturuki na Urusi ni washirika wawili katika ya pande mbili hasimu katika mzozo huo.

Nchi hizo mbili zinaunga mkono kambi mbili zinazokinzana nchini Libya. Moscow inaunga mkono mbabe wa kivita mashariki mwa Libya, Marshal Haftar, wakati Ankara ikiunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa yenye makao makuu jijini Tripoli, na kambi ya Magharibi mwa Libya kwa ujumla. Nchi zote mbili hizi zimetuma idadi kubwa ya silaha na maelfu ya wanajeshi nchini Libya. Wapiganaji wanaojulikana kwa jina la "Wagner" na vile vile mamluki kutoka Syria wanaounga mkono Urusi, mamluki kutoka Syria na mataifa mengine mengi kwa upande wa Uturuki wako nchini Libya kusaidia pande mbili hasimu katika vita hivyo.

Kwa hiyo Urusi na Uturuki zinashindana nchini Libya kama vile nchini Syria. Kila nchi inatafuta kuongeza ushawishi wake, huku ikijaribu kutafuta maelewano, bila hata hivyo kufanikiwa.

Mwezi Juni, Mawaziri wa Mambo ya nje na Ulinzi wa Urusi walipana ziara nchini Uturuki, lakini ilifutwa katika dakika za mwisho wakati mazungumzo yalilenga kusitisha vita. Wakati huo Urusi ilibaini kile ilichokiita kutokea kwa "tofauti kubwa".

Leo, baada ya duru mbili mpya za mazungumzo mweziJulai na Agosti, hatua inaonekana imepigwa kuhusiana na utaratibu wa kutekeleza usitishaji vita. Ujumbe wa pamoja utasafiri kwenda Libya kufafanua sehemu za kujitoa kwa pande mbili karibu na mji wa Sirte. Tume ya pamoja ya uratibu kuhusu Libyapia itaundwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.