Pata taarifa kuu
TUNISIA-IS-USALAMA

Tunisia: Kundi la Islamic State ladai kutekeleza shambulio lililoua afisa wa polisi

Kundi la Islamic State (IS), kupitia shirika lake la propaganda AMAQ, limekiri kuhusika na shambulio lililogharimu maisha ya afisa mmoja wa kikosi cha ulinzi wa taifa jana Jumapili huko Sousse, mji wa kitalii Mashariki mwa Tunisia.

Polisi wa Tunisia wanafanya uchunguzi kwenye eneo la shambulio dhidi ya maafisa wa kikodsi cha ulinzi wa taifa  Septemba 6, 2020 huko Sousse, Tunisia.
Polisi wa Tunisia wanafanya uchunguzi kwenye eneo la shambulio dhidi ya maafisa wa kikodsi cha ulinzi wa taifa Septemba 6, 2020 huko Sousse, Tunisia. AFP
Matangazo ya kibiashara

IS imetaka kutangaza kifo cha afisa mmoja wa vikosi vya usalama katika shambulio lililofanywa na "wapiganaji" wa skundi hilo, bila hata kutoa maelezo zaidi.

Jumapili mapema asubuhi, watu waliokuwa kwenye gari waliwavizia maafisa wa kikosi cha ulinzi wa taifa karibu na eneo lililo karibu na bandari ya Kantaoui, katika mji wa kitalii wa Sousse, kisha wakawashambulia kwa kisu, na kumuua mmoja wao na kumjeruhi vibaya mwengine.

Wauaji watatu, ikiwa ni pamoja na ndugu wawili, waliuawa Jumapili asubuhi katika eneo hilo hilo. Hawakuwa wanakujulikana na mamlaka nchini Tunisia.

Watu saba pia walikamatwa kuhusiana na uchunguzi huo, ikiwa ni pamoja na mke wa mmoja wa washambuliaji, ndugu wawili na mtu mmoja anayeshukiwa kuwa msajili, kimebaini kikosi cha ulinzi wa taifa.

Shambulio hili jipya dhidi ya vikosi vya usalama, katika jiji ambalo moja ya mashambulizi mabaya ya kijihadi ambayo yaliikumba nchi hiyo mwaka 2015, lilitokea siku tatu baada ya serikali mpya kuapishwa, baada ya mvutano mkali wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.