Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi yaongezeka Madagascar

Wakuu wa hospitali za mji mkuu wa Madagaskar, Antananarivo, wanasema idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona imeendelea kuongezeka licha ya kusambazwa kwa dawa ya mitishamba iliyootolewa na rais wa nchi hiyo kama tiba dhidi ya virusi vya Covid 19.

Wataalam wa maabara ya Chuo Kikuu cha Pasteur huko Madagascar wakifanya vipimo vinajulikana kama "PCR" ili kuona ikiwa wagonjwa wameambukizwa virusi vya Covid-19. Aprili 23, 2020, huko Antananarivo.
Wataalam wa maabara ya Chuo Kikuu cha Pasteur huko Madagascar wakifanya vipimo vinajulikana kama "PCR" ili kuona ikiwa wagonjwa wameambukizwa virusi vya Covid-19. Aprili 23, 2020, huko Antananarivo. RIJASOLO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Licha ya ugavi wa dawa ya mitishamba inayotokana na mmea wa Artemisia iliosambazwa na rais wa nchi hiyo Andy Rajoelina dhidi ya Virus vya Corona idadi ya maambukizi imeongezeka zaidi kiasi cha hopitali nchini humo kuzidiwa.

Licha ya rais huyo kuthibitisha kuwa dawa hiyo inatibu virusi vya Corona, hakuna wataalamu wowote waliothibitisha hilo, na hata shirika la Afya Duniani haikuwahi kuthibitisha hilo.

Licha ya ugavi wa dawa ya mitishamba inayotokana na mmea wa Artemisia iliosambazwa na rais wa nchi hiyo Andy Rajoelina dhidi ya Virus vya Corona idadi ya maambukizi imeongezeka zaidi kiasi cha hopitali nchini humo kuzidiwa.
Licha ya ugavi wa dawa ya mitishamba inayotokana na mmea wa Artemisia iliosambazwa na rais wa nchi hiyo Andy Rajoelina dhidi ya Virus vya Corona idadi ya maambukizi imeongezeka zaidi kiasi cha hopitali nchini humo kuzidiwa. REUTERS/Gertruud Van Ettinger

Madaktari katika hospitali kuu za Antananarivo, wanasema vitanda vinaanza kujaa wagonjwa wa Covid-19.

Nasolotsiry Raveloson mkurugenzi wa hospitali ya Andohotapenaka iliotengwa maalum, wakati wa janga hilo, kuwapokea wagonjwa wa Covid-19 amesema kwa sasa hawapokei tena mgonjwa wa Covid-19 ispokuwa pekee wagonjwa wenye hali mbaya. Hali kama hiyo inaripotiwa pia katika Hospital ya Chuo Kikuu Anonsiala na ile ya Josephe Raseta Befelatanana

Madagascar imeorodhesha rasmi kesi 7,548 za Covid-19, pamoja na vifo 65, lakini kwa siku kadhaa, nchi hiyo imeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya kesi za maambukizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.