Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA-SIASA

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu mataifa yanayoingilia katika mzozo wa Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mataifa ya kigeni kuendelea kuingilia mzozo wa Libya, kumefikia katika hali isiyokubalika.

Vita vinaendelea kurindima nchini Libya.
Vita vinaendelea kurindima nchini Libya. Abdullah DOMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Guteress ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa hali inaendelea kuwa mbaya nchini Libya kwa kuendelea kushuhudiwa ongezeko la kutumwa silaha na mamluki kutoka nchi za nje.

Kufikia sasa mataifa kadhaa yameendelea kuhusika katika vita vinavyoendelea nchini Libya. Urusi, Sudan na Chad wanasaidia vikosi vya Marshal Khalifa Haftar (LNA).

Mamluki kutoka Uturuki na maelfu ya raia wanaojiolea kutoka Syria wametumwa na Uturuki kusaidia wanamgambo walio waaminifu kwa serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) inayoongozwa na Fayez el-Sarraj.

Hivi karibuni Ufaransa ilistumu Uturuki kuingiza silaha nchini Libya .

Libya imekosa Amani tangu mwaka 2011 baada ya kuuawa kwa kiongozi wa wakati huo Muamar Kadhafi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.