Pata taarifa kuu
AFRIKA-WTO-BIASAHARA

Afrika yawakilishwa na wagombea watatu katika uchaguzi wa mkuu wa WTO

Serikali ya Kenya imemteua waziri wa michezo  Amina Mohammed kuwania kiti cha mkuu wa  shirika la dunia la  kibiashara WTO. Wadadisi wanasema huenda Afrika ikapoteza nafasi hiyo kutokana na kuwa imegawanyika kwa kumteuwa mtu mmoja kuwania kiti hicho.

Amina Mohamed, Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Kenya, ambaye ni mgombea kwenye nafasi ya mkuu wa WTO.
Amina Mohamed, Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Kenya, ambaye ni mgombea kwenye nafasi ya mkuu wa WTO. wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mohammed anawania kiti hicho kwa mara ya pili baada ya kushindwa mwaka 2013 na anatazamiwa kupambana na wagombeaji wengine watano kutoka Mexico,Moldova, Nigeria, Misri na Korea Kusini.

Nigeria imemteua mchumi wa nchi hiyo Dr. Ngozi Okonjo-Iweala kugombea nafasi ya mkurugenzi mkuu mpya wa WTO. Dk. Okonjo-Iweala kwa sasa ni mwenyekiti wa Baraza la muungano wa chanjo la Dunia. Katika kipindi cha mlipuko wa virusi vya Corona, akiwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika, ameshughulikia kukusanya fedha za kimataifa kuunga mkono mapambano dhidi ya virusi hiyo.

Misri pia imemteua mtaalamu wake wa sheria Abdel-Hamid Mamdouh kugombea nafasi ya mkurugenzi mkuu wa WTO. Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na serikali ya Misri, Mamdouh ana uzoefu na ujuzi mkubwa katika sera na mazungumzo ya kibiashara.

Umoja wa Afrika ulikuwa umepanga kuwa na mgombea mmoja atakayeungwa mkono na nchi zote za Afrika ili kuwa na bahati ya kushindia nafasi hiyo, lakini hilo halijafanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.