Pata taarifa kuu
DRC-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi DRC yafikia 3,494

Idadi  ya watu wanaoambukizwa virusi vya Corona inaendelea kuongezeka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.  Kufikia sasa DRC imerekodi visa 3,494 vya maambukizi ya virusi vya Corona. 

Kituo cha kupima virusi vya Corona, Kinshasa, DRC.
Kituo cha kupima virusi vya Corona, Kinshasa, DRC. Freddy Tendilonge/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wagonjwa 492 wamepona, huku watu 74 wakithibitishwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Kinshasa ndio kitovu cha ugonjwa huu hatari. Kituo cha kupima kwa bure virusi vya Corona kimejengwa tu kwa kipindi cha wiki tatu. Ni kituo cha kwanza kutengwa na idara ya kitaifa ya kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa Covid-19, INRB, inayoungwa mkono na Shirika la Afya Duniani, WHO.

Kituo hicho kilichotengwa kwenye uwanja wa mpira wa mguu wa Martyrs jijini Kinshasa ni kituo cha kwanza kupima bure watu virusi vya Corona. Kituo hicho kilijengwa kwa lengo lakudhibiti janga la Covid-19.

“Kwanza tunawapima joto, kisha tunafanya vipimo vya maabara, sampuli inachukuliwa kwenye makamasi ndani ya tundu za pua na mate. Kila mutu anatakiwa kuacha vitambulisho vyake uraia, ili wakati tutamaliza zoezi la kupima tuwajuze kama wana maambukizi ya Corona au la,” amesema Laurent Ndunge, mwakilishi wa taasisi ya kukabiliaana najanga mchini INRB.

Wakati raia wengi wakiwa na hofu ya kupima, baadhi ya raia, wameonyesha umuhimu wakujua hali ya Afya zao.

Zaidi ya vipimo 500 vimefanyika tangu kituo hiki kuanzishwa Mei 18 mwaka huu.

Kituo cha kupima virusi vya Corona huko Kinshasa.
Kituo cha kupima virusi vya Corona huko Kinshasa. Freddy Tendilonge/RFI

DRC inaendelea kukumbwa na milipuko miwili ya magonjwa hatari kwa sasa, ikiwa ni pamoja na Covid-19 na Ebola. Ni kwa mara ya tatu DRC inakumbwa na ugonjwa huu wa Ebola uliozuka kwa mara ya kwanza nchini humo mwaka 1976.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.