Pata taarifa kuu
SOMALIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Mtu wa kwanza afariki dunia kwa Corona Somalia

Somalia imetangaza kifo cha kwanza kinachohusiana na ugonjwa hatari unaosumbua ulimwengu wa Covid-19 (Corona). Mtu aliyefariki dunia ni mwanaume, mwenye umri wa miaka 58, kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa Somalia, Fawziya Abikar.

Ugonjwa wa Covid-19 waendelea kuiathiri Somalia ambayo inaendelea kukumbwa na mashambulizi ya wanamgambo wa Al Shabab.
Ugonjwa wa Covid-19 waendelea kuiathiri Somalia ambayo inaendelea kukumbwa na mashambulizi ya wanamgambo wa Al Shabab. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Akiongea kupitia Twitter, Fawziya Abikar ametangaza kesi nne mpya za maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19, na kufanya idadi ya wagonjwa kufikia 12 nchini Somalia.

Ugonjwa wa Covid-19 (Corona) umesababisha vifo vingi duniani, huku Marekani ikiendelea kuathirika zaidi na ugonjwa huo.

Wagonjwa wa Corona sasa wamevuka 153, 000 duniani.

Mataifa kadhaa ya Afrika yimeweka mazuio ili kupambana na kuenea kwa virusi vya corona. Hatua hizo ni jaribio la kuzuia mlipuko wa virusi katika bara hilo lenye mifumo duni ya kiafya.

Benin, Liberia, Somalia na Tanzania ni nchi zilizoripoti kuwa na wagonjwa wa kwanza wa virusi hivyo.

Hivi karibuni shirika la Afya Duniani, WHO, ilionya kwamba "sasa virusi vya Corona vina dalili ya kuenea duniani kote."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.