Pata taarifa kuu
MAREKANI-SENEGAL-ANGOLA-USALAMA

Mike Pompeo aendelea na ziara yake Afrika

Baada ya Senegal Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo anaendelea na ziara yake nchini Angola. Hata hivyo uwepo wa askari wa Marekani barani Afrika bado uko mashakani. Hivi karibuni Marekani imetishia kuondoa askari wake barani Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo na mwenzake wa Senegal Amadou Ba katika mkutano na waandishi wa habari huko Dakar, Februari 16, 2020.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo na mwenzake wa Senegal Amadou Ba katika mkutano na waandishi wa habari huko Dakar, Februari 16, 2020. William de Lesseux/RFI
Matangazo ya kibiashara

Mikataba mitano ya kiuchumi imetiwa saini wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani huko Dakar. Maekani itajenga barabara kuu ambayo itaunganisha mji mkuu wa Senegal na Saint-Louis. Swala la usalama pia limejadiliwa, wakati ambapo Marekani inatathmini uwezekano wa kupunguza hatua kwa hatu askari wake katika Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Amadou Ba ameelezea masikitiko yake iwapo Marekani itahibitisha kuwa iko tayari kuondoa askari wake katika ukanda huo, huku akibaini kwamba Marekani ina mchango mkubwa kwa Afrika, hasa katika maswala ya usalama.

"Kwa kweli Marekani imetuambia nia yake ya kuondoa vikosi vinavyopigana, lakini hiyo haimaanishi kwetu kuondoka kwa vikosi vya Marekani. Tulizungumzakuhusu haja kuwepo kwa askari wa Marekani katika ukanda huu. Tunatumai kuwa Marekani itaendelea kutusaidia katika nyanja ya usalama, katika nyanja ya mafunzo, katika nyanja ya elimu," amesema Amadou Ba.

Mike Pompeo amebaini kwamba Pentagon inatathmini vizuri uwezekano wa kupunguza askari wa Marekani katika maeneo ya mizozo.

"Nina uhakika kwamba tutakapomaliza tathmini hii, tutajadili sio tu na Senegal, bali na nchi zote za ukanda huo. Tutazungumzia sababu za kile tunachofanya, njia tunayoitumia, na tutafikia matokeo ambayo yatamfurahisha kila mmoja," amesema Mike Pompeo.

Tumekuwa na majadiliano mengi kuhusu usalama wa kikanda, kuhusu jukumu la Marekani. Tutafanya kinachostahili. Tutafanya pamoja kinachostahili, nina uhakika na jambo hilo. Sina mengi ya kuongea, lakini Senegal inapaswa ifahamu kuwa, kwa pamoja, Senegal, vikosi vya ukanda, washirika wa Ulaya, Uaransa na sisi Marekani, tunalo jukumu la kurejesha usalama katika ukanda huu. Hii ndio sababu tunataka maendeleo ya uchumi wa nchi mbalimbali na nimeazimia kuendelea na njia hii. Nina hakika kwamba tutakapomaliza tathmini hii, tutaijadili, sio tu na Senegal, lakini nchi zote za ukanda huu, " ameongeza Mike Pompeo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema kuwa tishio la kigaidi katika Ukanda wa Sahel linaikabilia pia Marekani, huku akibaini kwamba mazungumzo yanaendelea na Senegal kwa kuendelea na mafunzo ya vikosi vya jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.