Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA-SIASA

Spika wa bunge la Libya aomba msaada kutoka nchi za Kiarabu

Baada ya kushindikana kwa mazungumzo jijini Moscow, nchini Urusi, Ujerumani inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa Januari 19 ili pande husika zisitishe mapigano nchini Libya na kuzindua tena mchakato huo.

Spika wa Bunge la Libya, Aguila Saleh, Bengaz, Aprili 13, 2019.
Spika wa Bunge la Libya, Aguila Saleh, Bengaz, Aprili 13, 2019. © Abdullah DOMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, mvutano unaendelea kushuhudiwa katika mji mkuu wa Libya Tripoli.

Hata hivyo hali ya utulivu inaendelea kutawala jijini Tripoli. Kila upande unajaribu kushikilia msimamo wake. Licha ya ukiukaji katika makubaliano ya kusitisha mapigano, hali bado ni tete nchini Libya.

Ili kuendelea kushikilia msimamo wake, kambi ya Khalifa Haftar imeongeza vikosi vyake katika maneo inayoshikilia, wakati vikosi vya Fayez el-Sarraj vinaendelea kutegemea msaada wa mamluki kutoka Syria, waliotumwa na Uturuki kusaidia serikali ya Tripoli. Wapiganaji elfu mbili kutoka Syria waliwasili jijini Tripoli katika wiki za hivi karibuni, kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Uingereza, The Guardian.

Wakati huo huo Spika wa Bunge la Libya, Aguila Saleh, Jumatano asubuhi wiki hii, alikuwa ziarani Cairo. Mbele ya Bunge la jumuiya ya nchi za Kiarabu, alithibitisha kwamba vikosi vinavyoongozwa na Marshal Khalifa Haftar, vitaendeleza na harakati zao na hivi karibuni vitaingia Tripoli ili kuikomboa kutoka mikononi mwa wanamgambo.

Aguila Saleh pia ametoa wito kwa nchi za Kiarabu kutotambua tena serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli inayoongozwa na Fayez el-Sarraj.

Spika wa Bunge la Libya pia alitoa wito kwa nchi za Kiarabu kuingilia kati ili kukabiliana na Uturuki ambayo imeingilia kijeshi nchini Libya.

Aguila Saleh amebaini kwamba mikataba miwili iliyotiliwa saini kati ya Ankara na serikali ya Fayez el-Sarraj ni kinyume cha sheria, kwani hawajapata idhini ya Bunge.

Katika taarifa, Bunge la jumuiya ya nchi za Kiarabu limelaani uamuzi wa Uturuki wa kupeleka vikosi nchini Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.