Pata taarifa kuu
LIBTA-RAMAPHOSA-SIASA-USALAMA

Ramaphosa: Nina wasiwasi kuhusu mgogoro wa Libya

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameelezea wasiwasi wake kuhusu mgogoro wa Libya, wakati akijiandaa kumrithi rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi kwenye uongozi wa Umoja wa Afrika.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa. © REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Bw Ramaphosa aliazungumza hayo alipokuwa akimpokea mgezi wake wa heshima, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ambaye alikuwa alikuwa amefanya ziara ya kiserikali nchini humo mwishoni mwa wiki hii.

Wawaili hao walijadili kuhusu uhusiano kati ya nchi zao mbili, lakini pia walijadili maswala mbalimbali kuhusu bara la Afrika.

Rais wa Afriak kusini Cyril Ramaphosa anajianda kuchukuwa mikoba ya rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sissi kama rais wa Umoja wa Afrika wakati wa mkutano wa kilele mwezi Februari.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Ethiopia alithibitisha kwamba Uchaguzi Mkuu utafanyika nchini mwake mwezi Mei au Juni.

Atakapochukuwa uongozi wa Umoja wa Afrika, Cyril Ramaphosa anatarajia kutafutia suluhu mgogoro wa Libya, ambao unaendelea kuiathiri nchi hiyo.

"Umoja wa Afrika umedhamiria kutokomeza vita katika nchi mbalimbali za bara hili, na Libya ni nchi ambayo ni muhimu sana barani Afrika kwa mpango wetu. Tunakaribisha tangazo la kusitisha mapigano, ambalo linatupa fursa ya kujenga suluhisho la amani. Tunapaswa tupate suluhisho kutoka nchi za Afrika kwa matatizo yanayozikabili nchi za Afrika, " Rais wa Afrika Kusini alisema.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed anatarajia kwamba Rais wa Afrika Kusini pia ataweza kuchangia katika mazungumzo katika mzozo kuhusu bwawa la Renaissance.

"Kama rafiki wa Ethiopia na Misri, kama ndugu, anaweza naweza kusimamia mazungumzo kati ya wadaui tofauti ili kusuluhisha tataizo hilo kwa amani, " amesema Abiy Ahmed.

Lakini Afrika Kusini haina picha nzuri kwenye bara la Afrika, baada ya wimbi la ghasia dhidi ya wageni waishio nchini humo zilizotokea mwezi Septemba mwaka jana.

Hata hivyo rais wa Afrika Kusini amehakikisha kwamba "serikali ya Afrika Kusini iko wazi kabisa kwa swala hilo.

"Wale wote ambao wapo Afrika Kusini wanakaribishwa, na kamwe hawapaswi kushambuliwa na mtu yeyote, " Bw Ramaphosa amebaini.

Rais pia anatarajia kutumia mamlaka yake kwenye uongozi wa Umoja wa Afrika kuwezesha biashara kwa kukamilisha uanzishwaji wa eneo la biashara huria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.