Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Tshisekedi akumbwa na upinzani mkubwa kutoka Lamuka inayokumbwa na mgawanyiko

Wakati rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo akielekea kusherehekea mwaka 1 tangu hatamu ya uongozi wa nchi, joto la kisiasa linaendelea kuikumba nchi hiyo.

Felix Tshisekedi wakati wa hotuba yake, Kinshasa Desemba 13, 2019.
Felix Tshisekedi wakati wa hotuba yake, Kinshasa Desemba 13, 2019. REUTERS/Hereward Holland
Matangazo ya kibiashara

Rais Tshisekedi anaendelea kukabilia na upinzani, huku baadhi ya wakosoaji wake ikiwa ni pamoja na mpinzani wake mkuu Martin Fayulu wakiendelea kupinga uongozi wake.

Akiwa katika mji wa kikwiti, Martin Fayulu, mpinzani wa serikali amesema mwaka 2020 ni mwaka wa ukombozi wa Congo, huku akitangaza maandamano ya amani kuanzia Januari 17 kukumbuka mauaji ya baba wa taifa nchini Congo Emery Patrice Lumumba.

Kupitia maandamano hayo, mgombea huyo ambae alishindwa katika uchaguzi wa urais uliopita anatarajia kukemea kile alikichoita mpango wa Kabila juu ya ukandamizaji wa nchi.

Upande wake Adolphe Muzito, mratibu mpya wa muungano wa Lamuka, amesema Fayulu ndie rais mteule wa Jamhuri na ametoa wito kwa waandamanaji kuvalia kitambaa cheupe kichwani, ishara ya kuomboleza "kuashiria ghadhabu ya mauaji huko Beni".

Lakini ndani ya jukwaa hilo la Lamuka, mtazamo huu haugwi mkono na wote. Moïse Katumbi na Jean-Pierre Bemba wanasema wanashangazwa na tamko hili ambalo haikuwa mada ya mashauriano.

Migongano, na mizozo, imejitokeza katika familia hii ya kisiasa ya wapinzani tangu uchaguzi wa Félix Tshisekedi. Moïse Katumbi hivi karibuni ameunda chama chake Ensemble pour la République, na kutangaza kuwa ni mpizani wa wastani msimamo ambao unaonekana pia kuungwa mkono na Jean-Pierre Bemba na chama chake, MLC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.