Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Burkina Faso: Polisi ya Djibo yakumbwa na shambulizi jipya

Vikosi vya usalama katika eneo la Djibo, katika mkoa wa Soum, Kaskazini mwa Burkina Faso vimekumbwa na shambulizi jipya usiku wa kuamkia Jumatano Desemba 31. Afisaa moja wa polisi ameuawa katika shambulizi hilo.

Askari wa Burkina Faso wakati wa mazoezi ya kupambana na ugaidi mashariki mwa nchi, Aprili 13, 2018 (picha ya kumukumbu).
Askari wa Burkina Faso wakati wa mazoezi ya kupambana na ugaidi mashariki mwa nchi, Aprili 13, 2018 (picha ya kumukumbu). AFP PHOTO/ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Burkina Faso vinaendelea kukabiloiwa na mashambulizi ya makundi ya kigaidi. Eneo la Djibo linaendelea kushuhudia mdororo wa usalama kwa miezi kadhaa.

Mashahidi wanasem akundi la watu kadhaa wenye silaha waliendesha shambulio dhidi ya kambi ya polisi katika eneo la Djibo. Kwa mujibu wa chanzo cha polisi, washambuliaji hao walilazimika kutimka baada ya kuwasili kikosi cha polisi waliokuja kusaidia.

Mwezi Oktoba 2018, watu kadhaa wenye silaha walivamia kambi hiyo. Katika shambulio hilo magari kadhaa yalichomwa moto, silaha nyingi zilibiwa na wafungwa wengi walitoroka. Mwezi Novemba mwaka jana, meya wa Djibo aliuawa.

Kwa miezi kadhaa magaidi wamekuwa wakijaribu kudhibiti makao makuu ya manispaa ya jiji hilo. Kwanza walijaribu kutenganisha mji huo na miji mingine kwa kuharibu barabara muhimu, huku wakiharibu pia Daraja la Boukouma, mashariki mwa mji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.