Pata taarifa kuu
CAR-CHAD-HAKI

Kiongozi wa waasi Jamhuri ya Afrika ya Kati Miskine aendelea kuzuiliwa Chad

Mamlaka nchini Chad haina uwezo wa kumsafirisha Abdoulaye Miskine na wenzake kwenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kujibu shutma zinazowakabili, kwa mujibu wa vyanzo kutka Chad.

Kiongozi wa waasi wa FDPC Abdoulaye Miskine na wapiganaji wake huko Biti.
Kiongozi wa waasi wa FDPC Abdoulaye Miskine na wapiganaji wake huko Biti. © FDPC / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hayo yamethibitishwa na wanasheria wa kiongozi wa chama cha waasi cha People Democratic Front, kiliyotia saini kwenye mkataba wa amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na waasi katika mji mkuu wa Sudani, Khartoum.

Abdoulaye Miskine na wenzake walikamatwa siku kumi zilizopita wakati waliingia nchini Chad baad aay kuvuka mpaka kati ya nchi hiyo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kwa mujibu wa wanasheria wa Abdoulaye Miskine, walikuja nchini Chad kuomba serikali ya nchi hiyo kuwa mpatanishi katika mgogoro nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuhusu utekelezwaji wa mkataba wa amani wa Khartoum uliofikiwa mwezi Februari mwaka huu.

Kwa bahati mbaya, hawakusikilizwa lakini walikamatwa, na tangu wakati huo wameendelea kuzuiliwa kinyume cha sheria, amesema Maxvelt Loalngar, mmoja wa mawakili wao.

"Makubaliano kati ya nchi wanachama wa Cemac yanabaini kwamba Baada ya saa 72 raia wa kigeni anayezuiliwa katika ardhi ya Chad, anapaswa kuachiliwa huru, " amebaini Maxvelt Loalngar.

"Mpaka sasa, hatuwezi kumuona Abdoulaye Miskine na wenzake. Hii inaonyesha kuwa wanazuiliwa kinyume cha sheria, na ni tusi kwa nchi yetu, " ameongeza wakili Loalngar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.