Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU-SIASA-USALAMA

Malalamiko yajitokeza baada ya uchaguzi Guinea-Bissau

Wananchi wa Guinea-Bissau wameshiriki kwa wingi katika uchaguzi wa urais katika mazingira yaliyotawaliwa na hofu na machafuko ya mitaani kwenye nchi hiyo maskini ya magharibi mwa Afrika.

Maafisa wa Tume ya uchaguzi nchini Guinea-Bissau wamebaini kwamba "mambo yamekamilika" kwa uchaguzi wa urais wa Jumapili.
Maafisa wa Tume ya uchaguzi nchini Guinea-Bissau wamebaini kwamba "mambo yamekamilika" kwa uchaguzi wa urais wa Jumapili. C.Idrac/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wagombea 12 wanachuana kwenye uchaguzi huo akiwemo rais wa hivi sasa, Jose Mario Vaz ambaye yuko madarakani tangu mwaka 2014.

Kwa mujibu wa Katiba ya Guinea-Bissau, uchaguzi huo utaingia kwenye duru ya pili iwapo atakosekana mgombea aliyepata zaidi ya asilimia 50 ya kura.

Wagombea wawili watakaopata kura nyingi zaidi watachuana tena tarehe 29 mwezi Desemba, iwapo wagombea wote 12 watashindwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura kwenye duru hii ya kwanza.

Guinea-Bissau ni koloni la zamani la Ureno, Ni nchi ndogo maskini ya magharibi mwa Afrika yenye watu milioni moja na nusu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.