Pata taarifa kuu
DRC

MONUSCO yatuma ndege tatu kusaidia utafutaji wa ndege ya DRC

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vinavyolinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vimetuma ndege tatu kusaidia kutafuta ndege ya mizigo ya serikali ya DRC iliyopotea tangu Alhamisi ikiwa na watu wanane ndani yake.

Rais wa DRC  Félix Tshisekedi
Rais wa DRC Félix Tshisekedi REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo, ambayo ilikuwa ikisambaza vifaa kwa ajili ya ziara ya Rais Felix Tshisekedi mjini Goma, ilipotea baada ya kuondoka Mashariki mwa nchi hiyo huku kukiwa na katika hali mbaya ya hewa.

Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO umepeleka ndege mbili na helikopta moja jana Jumamosi kujaribu kutafuta ndege hiyo Antonov 72, ambayo wafanyakazi wake ni pamoja na Warusi wawili kulingana na ubalozi wa Moscow jijini Kinshasa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.