Pata taarifa kuu
GAMBIA-HAKI

Gambia: Waathiriwa walipwa fidia kutoka mali ya Yahya Jammeh

Serikali ya Gambia imetoa euro 900,000 kwa mfuko wa misaada kwa waathiriwa wa utawala wa Dikteta Yahya Jammeh. Pesa hizo zimetoka kwa mali ya kiongozi huyo wa zamani wa Gambia, baada ya kukamatwa na serikali na kuuzwa.

Yahya Jammeh mwaka 2009.
Yahya Jammeh mwaka 2009. Β© REUTERS/Carlos Garcia Rawlins/Files
Matangazo ya kibiashara

Uuzaji wa mali ya Yahya Jammeh utaleta manufaa makubwa kwa Gambia. Yahya Jammeh alikuwa na mali zaidi ya 280, ikiwa ni pamoja na biashara na hifadhi za misitu au visiwa. Anashtumiwa pia kupitisha mlango wa nyuma karibu dola milioni 360 kutoka hazina ya serikali.

Waziri wa Sheria, Abubacarr Tambadou, amekaribisha hatua ya serikali ya kuwapa waathiriwa fedha zilizoibwa na Yahya Jammeh.

"Serikali inaamini kuwa kutumia utajiri na mali ya Yahya Jammeh kwa kulipa fidia wa waathiriwa wa utawala wake ndiyo njia bora na nzuri zaidi," waziri wa Sheria wa Gambia amesema.

Kwa upande wa Sheriff Kijera, kiongozi wa kituo cha kinachogudumia waathiriwa amesema serikali kukabidhi mali hizo kwa waathiriwa wa utawala wa Yahya Jammeh ni ushindi mdogo. Kwa muda mrefu amekuwa akifanya kampeni ili mali ya Yahya Jammeh itumike kwa kutoa fidia kwa waathiriwa. "Lakini huu ni mwanzo tu. Dalasi milioni hamsini [sawa na euro 900,000] haitoshi kulipa fidia kwa waathiriwa wote. Lakini mpango huu ni ishara nzuri iliyotumwa na serikali", amesema Sheriff Kijera.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.