Pata taarifa kuu
SENEGAL-HAKI-SIASA

Khalifa Sall aachiliwa huru baada ya msamaha wa rais

Rais wa Senegal Macky Sall ametoa msamaha kwa meya wa zamani wa Dakar, Khalifa Sall, ambaye alikuwa anazuiliwa tangu mwezi Machi 2017 na kuhukumiwa Agosti 2018 hadi kifungo cha miaka mitano.

Khalifa Sall, akiondoka gerezani, Septemba 29, 2019.
Khalifa Sall, akiondoka gerezani, Septemba 29, 2019. © JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya rais ilishapisha sheria ya kirais inayomuachila huru meya wa zamani wa Dakar na wenzake wawili, Mbaye Touré na Yaya Bodian, ambao walikuwa wanazuiliwa naye.

Khalifa Sall alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano na faini ya faranga za CFA milioni tano.

Alipatikana na hatia ya "kughushi katika maandishi ya kibiashara, kughushi katika hati za kiutawala na wizi wa fedha za umma".

Khalifa Sall, mwenye umri wa miaka 65, alichaguliwa meya wa Dakar mnamo mwaka 2009 na kuchaguliwa tena mnamo mwaka 2014, ni alijitenga na chama cha Kisoshalisti na chenye viti vingi kilicho mchagua Macky Sall mnamo mwaka 2012 na 2019.

Agosti 2018, sheria ya kirais ilimuwachicha kazi Khalifa Sall kama meya wa Dakar. Uamuzi huu ulichukuliwa siku moja baada ya Mahakama ya Rufaa ya Dakar kuthibitisha hukumu dhidi ya Khalifa Sall.

Bango kubwa lenye picha ya Khalifa Sall.
Bango kubwa lenye picha ya Khalifa Sall. © SEYLLOU / AFP

Mwanzoni mwa mwaka 2019, Mahakama Kuu ilitupilia mbali rufaa ya Khalifa Sall dhidi ya kifungo chake cha miaka mitano jela kwa ghushi hati za kiutawala na wizi wa mali ya umma.

Khalifa Sall, aliyechaguliwa mbunge katika uchaguzi wa wabunge mnamo mwaka 2017, hakuweza kushiriki hata siku moja katika kikao cha Bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.