Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-UGAIDI-KIBINADAMU

Jeshi la Nigeria lalifungia shirika la Action Against Hunger

Jeshi la Nigeria, limesitisha ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Action Against Hunger linayotoa misaada ya kibinadamu kwa madai kuwa ,linawapa hifadhi magaidi wa Boko Haram, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Wanajeshi wa Nigeria wanaopambana na Boko Haram, Kaskazini mwa nchi hiyo
Wanajeshi wa Nigeria wanaopambana na Boko Haram, Kaskazini mwa nchi hiyo AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo linadaiwa kuwapa hifadhi magaidi hao chakula na dawa.

Hata hivyo Shirika hilo limekanusha madai hayo, baada ya jeshi kufunga Ofisi zao mjini Maiduguri hata bila ya kuwapa taarifa.

“Action Against Hunger linasitisha shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu kwa mamilioni ya watu katika maeneo ya Maiduguri, Monguno na Damasak,”

“Hatua hii itahatarisha maisha ya watu wengi ambao watakosa misaada muhimu” Shirika hilo limesema kupitia kwa taarifa yake.

Madai ya Jeshi la Nigeria, limewashangaza wadau mbalimbali ambao wamesema hii ndio mara ya kwanza kwa tukio kama hili kutokea dhidi ya mashirika haya ya msaada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.