Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MUGABE-SIASA

Robert Gabriel Mugabe kuzikwa kijijini kwake Kutama Oktoba 15

Hatimaye Serikali ya Zimbabwe na familia ya Mugabe wameafikiana kuhusu mahala atakapozikwa Robert Gabriel Mugabe, kiongozi wa vita vya msituni alieongoza mapambano ya kukomesha utawala wa wazungu wachache katika nchi hiyo iliyokuwa inaitwa Rhodesia.

Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe Oktoba 2017.
Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe Oktoba 2017. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Familia ya rais huyo wa zamani Robert Mugabe imesema atazikwa mwanzoni mwa wiki ijayo nyumbani kwake Kutama, kaskazini-magharibi mwa mji wa Harare na sio kwenye makaburi ya kitaifa ya mashujaa wa ukombozi.

Mugabe alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na mwili wake uliwasili Jumatano wiki hii nchini Zimbabwe kutokea Singapore.

Kwa wakati huu raia wa Zimbabwe wanatoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe. Rais Emmerson Mnangagwa na maafisa wengine wa serikali wamefika nyumbani kwa rais huyo leo Alhamisi.

Mwili wa Mugabwe utaonyeshwa kwenye maeneo ya kihistoria kwa siku kadhaa.

Mugabe aliitawala Zimbabwe kuanzia uhuru mwaka 1980 hadi alipopunduliwa mwaka 2017.

Wakati wa utawala wake wa miaka 37, Zimbabwe iliporomoka kutoka taifa lililostawi hadi mgogoro wa kiuchumi.

Viongozi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Robert Gabriel Mugabe ikiwa ni pamoja na Rais wa China Xi Jinping, Rais wa zamani wa Cuba Raul Castro, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Mohammadu Buhari wa Nigeria na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.