Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA

Raia Sudani wasubiri kuundwa kwa Baraza Kuu litakalosimamia taasisi za mpito

Wananchi wa Sudani wamekuwa na shauku ya kujuwa majina ya watu watakaounda Baraza Kuu Tawala litakalosimamia taasisi za mpito nchini humo.

Ahmed al-Rabie, mwakilishi wa Alliance for Freedom and Change (kulia) na Mohammed Hamdan Daglo, kiongozi namba mbili wa Baraza la keshi (kulia akivalia sare ya jeshi, wakati wa kusaini makubaliano Agosti 17, 2019.
Ahmed al-Rabie, mwakilishi wa Alliance for Freedom and Change (kulia) na Mohammed Hamdan Daglo, kiongozi namba mbili wa Baraza la keshi (kulia akivalia sare ya jeshi, wakati wa kusaini makubaliano Agosti 17, 2019. AFP/Ebrahim HAMID
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo baadhi ya majina yameanza kutolewa. Lakini tangazo rasmi la kuundwa kwa baraza hilo (raia sita na wanajeshi watano) linatarajiwa kutolewa leo Jumatatu, Agosti 19.

Aisha Mousa, ni jina la mwanamke mmoja pekee ambaye atakuwa mmoja wa wajumbe wa Baraza hili Kuu Tawala, litakalosimamia taasisi za mpito kwa kipindi cha miaka tatu na miezi mitatu. Aisha Mousa alikuwa mstari wa mbele katika maandamano hayo yaliyoanza 19 Desemba kufuatia uamuzi wa serikali kuongeza mara tatu bei ya mkate.

Aisha Mousa ambae si maarufu nchini Sudani, anawakilisha wanawake wengi katika maandamano hayo. Miongoni mwa raia wengine wanne waliochaguliwa katika Baraza hili Kuu Tawala, ni profesa wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Khartoum, mmoja wa vigogo wa chama cha Ummah.

Kama ilivyoafikiwa, Baraza Kuu Tawala ambalo kwanza litaoongozwa na wanajeshi kwa miezi 21, halafu na raia, kwa miezi 18, halitakuwa na mamlaka mapana. Katika siku za usoni, Baraza hili litapitisha jina la Waziri Mkuu. Mchumi Abdalla Hamdok anapewa nafasi kubwa ya kuteuliwa nafasi hiyo. Waziri huyo mkuu atharakia kuteua serikali ya mpito ambayo itaanza kufanya kazi mara moja baada ya miezi mingi taifa hili likikumbwa na mvutano wa kisiasa. Kisha atakuwa na kazi ngumu ya kuweka sawa uchumi uliokumbwa na miezi kadhaa ya maandamano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.