TUNISIA-SIASA
Waziri Mkuu wa Tunisia kuwania kiti cha urais
Waziri Mkuu wa Tunisia na kiongozi wa chama cha Tahya Tounes Youssef Chahed, amewasilisha ombi la kuwania urais wakati wa uchaguzi utakaofanyika tarehe 15 mwezi ujao.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Leo Ijumaa imekuwa ni siku ya mwisho kwa wanasiasa kuwasilusha maombi yao na hatua ya Chahed, inamweka katika nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo.
Hata hivyo, anatarajiwa kupata ushindani kutoka kwa rais wa zamani Moncef Marzouki na Waziri wa Ulinzi Abdelkarim Zbidi.
Mshindi atamrithi rais wa zamani Beji Caid Essebsi, aliyefariki dunia mwezi uliopita akiwa na umru wa miaka 92.