Meya wa Mogadishu afariki dunia Doha, Qatar
Meya wa mji wa Mogadishu nchini Somalia, Abdirahman Omar Osman, amefariki dunia baada ya kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa muhanga lililoua watu sita juma lililopita mjini Mogadishu. Amefariki dunia mjini Doha, Qatar, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Imechapishwa:
Abdirahman Omar Osman alijeruhiwa wakati shambulio la kujitoa mhanga katika ofisi yake walipokuwa katika mkutano wa masuala ya usalama.
Abdirahman Omar Osman ambaye aliishi katika mji wa London nchini Uingereza baada ya kuitoroka nchi yake kufuatia kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, alirejea nchini Somalia mwaka 2008 kusaidia kuijenga upya nchi yake inayoendelea kukumbwa na mdororo wa usalama.
Katika ukurasa wa twitter, ujumbe wa Marekani nchini Somalia umemtaja bwana Osman kuwa ''mshirika mzuri sana na aliyekuwa akiwatumikia raia wa Somalia bila kuchoka''.