Pata taarifa kuu
DRC-NTAGANDA-ICC-HAKI

Hukumu dhidi ya Bosco Ntaganda kutolewa Julai 8

Mbabe wa zamani wa kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda, mwezi ujao atasimama mbele ya majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita, ICC, kujibu mashtaka ya tuhuma za kusimamia mauji na kuwatumia watoto kwenye jeshi lake la waasi.

Kiongozi wa wanamgambo wa DRC, Bosco Ntaganda, wakati kesi yake ikifunguliwa ICC, Hague, Uholanzi, Septemba 2, 2015.
Kiongozi wa wanamgambo wa DRC, Bosco Ntaganda, wakati kesi yake ikifunguliwa ICC, Hague, Uholanzi, Septemba 2, 2015. REUTERS/Michael Kooren
Matangazo ya kibiashara

Ntaganda ambaye alipewa jina la “Terminator”, anatuhumiwa kuhusika na kusimamia mauaji yaliyotekelezwa na wanajeshi wake dhidi ya raia kwenye jimbo la Ituri kati ya mwaka 2002 na 2003.

Ntaganda anakabiliwa na makosa 13 ya uhalifu wa kivita na matano ya uhalifu dhidi ya binadamu,  kwa ajili ya jukumu lake kwenye  mgogoro wa kikatili wa vita ya wenyewe kwa wenyewe katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zaidi ya miaka 15 iliyopita.

Ntaganda ambaye ana asili ya Rwanda, mnamo mwezi Septemba 2015 alikanusha kuhusika na uhalifu huo mwanzoni mwa kesi yake mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.

Waendesha mashitaka katika mahakama ya ICC iliyoko mjini the Hague, wanasema jeshi lake la waasi kati ya mwaka 2002 na 2003 lilifanya utawala wa hofu katika mkoa wa kaskazini mashariki wa Ituri, na kusababisha unyanyasaji wa kutisha dhidi ya wenyeji.

Ntaganda alipanga operesheni za jeshi lake la Patriotic Forces for the Liberation of Congo (FPLC), akiwatumia watoto kama askari na kuwalazimisha wanawake katika utumwa wa ngono, wakati akiwashambulia raia kwa misingi ya kikabila.

Mahakama ya ICC imesema hukumu dhidi ya kongozi huyo wa zamani wa waasi itatolewa Julai 8 mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.