Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA-WHO

Maambukizi ya Ebola yaendelea kuongezeka Mashariki mwa DRC

Wizara ya afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inasema watu zaidi ya 2,000 wameambukizwa ugonjwa hatari wa Ebola Mashariki mwa nchi hiyo tangu mwezi Agosti mwaka 2018.

Mgonjwa aliyeambukizwa Ebola akisaidiwa na maafisa wa afya Mashariki mwa DRC
Mgonjwa aliyeambukizwa Ebola akisaidiwa na maafisa wa afya Mashariki mwa DRC REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Kati ya watu hao, Wizara hiyo inasema watu 1,914 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo hatari.

Watu wengine 1,346 wamepoteza maisha huku wengine 539 wakipona baada ya kupata matibabu.

Siku za hivi karibuni, Wizara hiyo inasema maafisa wa afya wamejitahidi kutoa taarifa kuhusu namna ya kujizuia kupata ugonjwa huo, lakini watalaam wanaonya kuwa ni muhimu sana kuwepo kwa uangalifu mkubwa.

Visa vya maafisa na vituo vya afya kushambuliwa, pia vimepungua ikilinganishwa na miezi iliyopita.

Ugonjwa wa Ebola uligundulika katika Jimbo la Kivu Kaskazini tarehe 1 mwezi Agosti mwaka 2018 na ukasambaa katika hadi Ituri, lakini haujasambaa katika mataifa jirani.

Hii ni mara ya 10 kwa Ebola kuikumba nchi ya DRC, mara ya kwanza ikiwa mwaka 1976 na maambukizi haya ni mabaya baada ya yale yaliyoshuhudiwa katika nchi za Afrika Magharibi kati ya mwaka 2014-2016 na kusababisha vifo vya watu 11,300 hasa nchini Sierra Leone.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.