Pata taarifa kuu
DRC

DRC: Islamic State yawaachia huru mateka 22

Watu 22 waliokuwa wametekwa juma lililopita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika uvamizi uliofanywa na kundi la Islamic State, wameachiwa huru na watekaji wao.

Kofia ngumu ya askari wa DRC ikionekana ikiwa imetekelezwa kutokana na mapigano.
Kofia ngumu ya askari wa DRC ikionekana ikiwa imetekelezwa kutokana na mapigano. UN Photo/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kiongozi mmoja mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini, Donat Kibwana, amesema watu wote 22 waliachiwa wakiwemo wanaume 16, wanawake 5 na msichana mdogo.

Watu hao walitekwa nyara kwenye mji wa Samboko-Tchani Tchani juma lililopita.

Taarifa zaidi zinasema watekaji hao bado wanaendelea kuwashikilia watu wengine 6 wakiwemo watu watano wa familia moja.

Kibwana ameongeza kuwa watekaji walikuwa na miili tofauti kabisa na wenyeji wa eneo husika na walikuwa wakizungumza lugha ya kiswahili vizuri kama wanatoka eneo la Afrika mashariki (Tanzania).

Kwa mujibu wa tovuti ya Islamic State, kundi hilo limekiri kuhusika kwenye utekaji na kuongeza kuwa walishambulia kambi ya wanajeshi wa Serikali.

Mwezi uliopita, kundi la islamic State kwa mara ya kwanza lilikiri kuhusika katika utekaji na mashambulizi ya kambi ya jeshi kwenye jimbo la Kivu Kaskazini.

Mashambulizi kama haya yalizoeleka kutekelezwa na kundi jingine la kiislamu la ADF lenye asili ya Uganda na mara zote limekuwa likituhumiwa kuhusika na vitendo vya mauaji mashariki mwa DRC.

Kundi la ADF pia limekuwa likihusishwa na mauaji ya mamia ya watu yaliyotekelezwa mwaka 2014 kwenye mji wa Beni pamoja na utekaji nyara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.