Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA-MAANDAMANO

Waandamanaji wakaribisha makubaliano kati ya viongozi wao na jeshi Sudani

Waandamanaji nchini Sudan wamepokea kwa mikono miwili tangazo la kufikiwa makubaliano kati ya viongozi wao na wanajeshi wanaotawala kuhusu raia kushirikishwa kwenye Baraza la Kijeshi, hatua inayotoa njia ya kuelekea kuundwa kwa Serikali ya kiraia.

Mbali na kutimuliwa na kukamatwa kwa Omar al-Bashir, waandamanaji wanaendelea kukusanyika mbele ya makao makuu ya jeshi Khartoum.
Mbali na kutimuliwa na kukamatwa kwa Omar al-Bashir, waandamanaji wanaendelea kukusanyika mbele ya makao makuu ya jeshi Khartoum. OZAN KOSE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano haya yanamaanisha kuwa Baraza la Kijeshi sasa litalazimika kuundwa na idadi sawa ya raia katika kuendelea mbele na mazungumzo ya mchakato wa uundwaji wa Serikali.

Chini ya makubaliano haya jeshi litabaki kuwa muangalizi mkuu wakati raia watahusika na uendeshaji wa shughuli za kila siku za Serikali.

Siku ya Jumatano jioni wiki jana, pande hizi mbili ziliafikiana kuunda kamati ya pamoja ili kutatua tofauti zao.

Wiki iliyopita maafisa watatu ambao ni miongoni mwa viongozi wakuu wa Baraza la Kijeshi la Mpito walijiuzulu baada ya kushtumiwa kuwa na ushirikiano wa karibu na utawala uliopinduliwa. Mafisa hao ni Jenerali Zineladine, mkuu wa kamati ya kisiasa ya Baraza la Kijeshi, na maafisa wengine wawili, ikiwa ni pamoja na mkuu wa polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.