Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Vita vya Libya vyaibuka kwenye mitandao ya kijamii

Ikiwa mapigano yanaendelea kurindima na kushika kasi kusini mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli, tangu majeshi ya Marshal Khalifa Haftar kuzindua mashambulizi kwa lengo la kuteka mji huo, vita hivi pia vinaendelea kuibuka kwenye mitandao ya kijamii.

Mtu huyu akiangalia simu yake ya mkononi kwenye mabonde ya ziwa la Julai 23, katikati mwa mji wa Benghazi, mashariki mwa Libya,  Aprili 6, 2019.
Mtu huyu akiangalia simu yake ya mkononi kwenye mabonde ya ziwa la Julai 23, katikati mwa mji wa Benghazi, mashariki mwa Libya, Aprili 6, 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa raia, Facebook ni njia ya kwanza ya kupata habari, bila hata hivyo kuwa na uhakika wa habari halisi.

Na kambi mbili hasimu zinazopigana katika vita hivyo zinaelewa kuwa mtandao wa kijamii ni silaha kubwa katika vita hivyo vinavyoendelea nchini Libya.

Aidha, kwenye uwanja wa vita, wakati mwingine wapiganaji wanashikilia silaha na wengine kuwapiga picha.

Wiki iliyopita, Kanali Mohamad Gnounou, msemaji wa vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa (GNA) alishtumu vikosi vya Marshal Khalifa, kuweza kuingia sehemu ya mji na kupiga pichana baadae kuondoka na kurudi kwenye ngome zao. Na kisha wanatangaza kwamba wamedhibiti maeneo yaliyo karibu na kambi ya jeshi au eneo fulani, na wakati si kweli, amesema Kanali Gnounou.

Hata hivyo mapigano bado yanaendelea pembezoni mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli. Baadhi ya raia wa maeneo hayo wametoroka makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.