Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA-MAANDAMANO

Waandamanaji waapa kuendelea na maandamano Sudani

Waandamanaji nchini Sudani wameapa kuendelea na maandamano saa chache baada ya jeshi kuchukuwa hatua ya kumtimua rais Omar al-Bashir kwenye wadhifa wake na kuchukuwa madaraka.

Umati wa wa watu ukimiminika mitaani katika mji mkuu wa Sudani, Khartoum, kabla ya kutimuliwa kwa rais Omar el-Bashir, Alhamisi, Aprili 11, 2019.
Umati wa wa watu ukimiminika mitaani katika mji mkuu wa Sudani, Khartoum, kabla ya kutimuliwa kwa rais Omar el-Bashir, Alhamisi, Aprili 11, 2019. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wanasema Baraza la jeshi lililoundwa ni sehemu ya utawala uliong'olewa madarakani.

Rais Omar al-Bashir alipinduliwa na kukamatwa siku ya Alhamisi baada ya miezi kadhaa ya maandamano.

Waandamanaji wameliita Baraza la jeshi kuwa ni muendelezo wa utawala ulio kuwepo na kusema kuwa wataendelea kupambana na kupinga kwa amani.

Hata hivyo taarifa rasmi iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali vilisema kuwa tahadhari ya kutotoka nje itaanza kutekelezwa kuanzia saa nne za usiku siku ya Alhamisi Aprili 11 majira ya Sudan.

Bwana Bashir anakambiliwa na kibali cha kukamtwa kilichotolewa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC), ambayo inamshutumu kwa kupanga uhalifu wa kiviuta na uhalifu dhidi ya binadamu katika jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur.

Waziri wa Ulinzi Awad Ibnouf amesema, jeshi litaongoza kwa kipindi cha mpito, kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi mpya na kupatikana kwa Katiba mpya.

Aidha, Ibnouf ameeleza kuwa mbali na hatua hiyo, "hali ya hatari itashuhudiwa nchini humo kwa muda wa miezi mitatu kati ya saa nne usiku hadi saa 10 Alfajiri".

"Wafungwa wote wa kisiasa wanatarajiwa pia kuachiliwa huru, baada ya tangazo hili" , ameongeza Bw Ibnouf.

Wakati huo huo Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya, Ufaransa, Marekani, Ujerumani na Uingereza wamelaani jaribio la mapinduzi nchini Sudani wakisema kuwa Omar al-Bashir na serikali yake wamechaguliwa kidemokrasia, na hivyo kulitaka Baraza la jeshi kukabidhi madaraka kwa raia haraka iwezekanavyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.