Ushindi wa Azali Assoumani wathibitishwa
Mahakama ya kikatiba nchini Comoro imethibitisha ushindi wa rais Azali Assoumani baada ya kupata asilimia 59 ya kura zote, katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi uliopita.
Imechapishwa:
Hata hivyo, upinzani umekataa ushindi wake na kusema aliiba kura na hivyo hauwezi kumtambua kama rais wa Comoro.
Siku ya Jumanne rais Azali Assoumani amelihutubia taifa akiwa na ujumbe wa kujaribu kuwaunganisha wananchi wa taifa hilo, na kuwataka wapinzani kufungua ukurasa mpya na kukubali matokeo.
Upinzani chini ya vuguvugu la CNT ulikuwa umeahidi kuanzisha kampeni za vurugu nchini humo, huku waziri wa mambo ya ndani naye akiahidi kutekeleza sheria iwapo kutatokea vurugu.