Pata taarifa kuu
CAMEROON-SIASA-UPINZANI

Kiongozi wa upinzani nchini Cameroon ahojiwa

Kiongozi mkuu wa Upinzani nchini Cameroon Maurice Kamto amehojiwa na polisi wa mahakama  ikiwa ni Siku mbili baada ya kumkamatwa akiwa nyumbani kwa mmoja wa wafuasi wake huko Douala, mgombea huyo wa zamani wa kiti cha urais bado anaendelea kushikiliwa huko Yaoundé.

Kiongozi wa upinzani nchini Camaeroon Maurice Kamto
Kiongozi wa upinzani nchini Camaeroon Maurice Kamto AFP/MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Mashtaka dhidi ya Maurice Kamto ni mazito: anatuhumiwa kuunda kikundi cha uasi, uadui dhidi ya nchi, kuhmasisha umma kuasi, kosa ikiwa ni kosa kubwa zaidi ya yote yaliyowasilishwa Jumatano alasiri.

Mamlaka pia inawatuhumu wafuasi wa chama chake cha MRC, na kuwataka kuwajibika kutokana na uharibifu dhidi ya balozi za Cameroon huko Paris na Berlin Jumamosi iliyopita.

Zaidi ya watu 100 wafuasi wa mgombea huyo wa zamani wa kiti cha urais wanazuiliwa katika maeneo mbalimbali nchini Cameroon ambapo baadhi wamesikilizwa pia.

Umoja wa Mataifa na shirika linalo tetea haki za Binadamu la Human Right Watch wamebaini wasiwasi wao kuhusu hali inayoendelea nchini Cameroon na kuwatolea wito viongozi wa nchi hiyo kuheshimu uhuru wa kujieleza wakati huu waandishi wa habari wawili wakizuiliwa sambamba na walichokiandika kuhusu maandamano ya mwishoni mwa juma.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.