Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Uchaguzi DRC: Jina la mrithi wa Kabila bado lasubiriwa

Raia na wanadiplomasia wanaongeza shinikizo kwa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutangaza matokeo ya uchaguzi uliofanyika Desemba 30 mwaka jana kuziba nafasi ya rais Joseph Kabila anayemaliza muda wake.

Kurazaendelea kuhesabiwa katika baadhi ya maeneo DRC.
Kurazaendelea kuhesabiwa katika baadhi ya maeneo DRC. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa ni zaidi ya juma moja sasa tangu kufanyika kwa uchaguzi huo, Tume Huru ya Uchaguzi nchini DRC, CENI, bado haijaweka wazi ni lini hasa itatangaza matokeo rasmi ingawa kuna uwezekano wa kutangaza juma hili.

Mwishoni mwa juma mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC, Corneille Nangaa aliwataka wananchi kuwa watulivu huku akikataa kufanya kazi kwa shinikizo la wanasiasa au jumuiya ya kimataifa.

Katika maeneo kadhaa kura zinaendelea kuhesabiwa hasa katika maeneo kadaa ya mkoa wa Kivu ya Kusini, hususan Uvira na maeneo ya Tanganyika.

Tarehe mpya ya kutangazwa kwa uchaguzi haijajulikana. Lakini Tume Huru ya Uchaguzi imesema inafanya kila lililo chini ya uwezo wake ili iweze kutangaza matokeo ya uchaguzi haraka iwezekanavyo kabla ya tarehe 18 Januari 2019, tarehe ambayo ilipangwa kutawazwa kwa rais mpya.

Raia wa DRC walikuwa wamesubiri kutolewa kwa matokeo hayo, siku ya Jumapili Januari 6 kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa imetangazwa hapo awali na Tume ya Uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Corneille Nangaa amesema siku ya Jumapili, haikuwezekana kutangazwa matokeo hayo kwa sababu mchakato huo bado haujapatikana.

Mapema wiki hii amesema Tume ya uchaguzi imeshahesabu asilimia 50 ya kura zilizopigwa.

Ushindani mkali unashuhudiwa kuwa kati ya mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary, Martin Fayulu na Felix Tshisekedi wote kutoka upande wa upinzani.

Upinzani unaona kuwa kuchelewa kutangaza matokeo ya uchaguzi ni mbinu za kutaka kuiba kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.