Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DRC-JOSEPH KABILA-CENI

Kwanini uchaguzi wa DRC ulioshindwa kufanyika 2016, unafanyika 2018?

Uchaguzi unaofanyika leo, ulitarajiwa kufanyika mwaka 2016, baada ya muda wa rais Joseph Kabila kumalizika, lakini haikuwa hivyo, ni kwanini uchaguzi huu umekuwa ukiahirishwa ?

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC, Corneille Nangaa
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC, Corneille Nangaa REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu ulitarajiwa kufanyika mwishi wa mwezi Desemba mwaka 2016 lakini, Tume ya Uchaguzi ilitangaza kwa sababu ya kutomalizika kwa zoezi la kuwasajili wapiga kura lakini pia usalama hasa katika jimbo la Kasai, usingemalizika.

Uchaguzi huo uliahirishwa kwa mwaka mmoja zaidi hadi mwezi Desemba mwaka 2017, na wakati huo ulipofika, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Corneille Nangaa, alitangaza kuwa kuendelea kwa machafuko hasa kule Kasai, zoezi la kuwasajili wapiga kura lisingefanyika.

Mbali na suala ya usalama, serikali ya DRC ilikuwa inasema kuwa haikuwa na fedha za kuandaa Uchaguzi huo na wakati huo wote, waandamanaji wa upinzani walikuwa wanaandamana kushinikiza kujiuzulu na kufanyika kwa uchaguzi huo.

Hatimaye, ilikubaliwa kuwa uchaguzi ungefanyika tarehe 23 mwezi Desemba mwaka 2018, lakini suala tata lilikuwa ni matumizi ya mashine ya kupigia kura, wanasiasa wa upinzani waliendelea kushukuwa kuwa mashine hizo zinalenga kuiba kura.

Siku chache kuelekea uchaguzi wa tarehe 23, CENI iliahirisha Uchaguzi huo hadi tarehe 30 baada ya kuteketea kwa jengo la kuhifadhi vifaa vya kupigia kura jijini Kinshasa.

CENI haikuishia hapo, wiki hii, ilitangaza kuahirisha uchaguzi wa leo hadi mwezi Machi mwaka 2019 katika maeneo ya Beni, Butembo na Yumbi kwa sababu za Ebola na usalama.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.