Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Historia ya siasa ya DRC yaanza baada ya uhuru

Safari ya DRC ya kisiasa na uongozi imekuwa tangu ilipopata uhuru mnamo mwaka 1960. Baada ya kupata uhuru mwaka 1960, ilikubaliwa kuwa baba wa demokrasia nchini humo Patrice Lumumba awe Waziri Mkuu huku Jospeh Kasa Vubu akiwa rais wa kwanza.

Ramani ya DRC
Ramani ya DRC RFI.
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, baada ya kuwa katika nafasi hiyo kwa muda mfupi na kutofautiana na wenzake kuhusu mzozo wa kisiasa kuhusu mikoa ya Katanga iliyokuwa inataka kujitawala, aliuawa mwaka 1961.

Wanahistoria wanasema kuuawa kwa Lumumba, ndio chanzo cha mzozo wa muda mrefu wa taifa hilo ambao bado unashuhudiwa mpaka hivi sasa.

Mwaka 1965, Mobutu Sese Seko ambaye alikuwa Mkuu wa Majeshi, aliongoza mapinduzi ya kijeshi na kuchukua uongozi wa taifa hilo, na kukaa madarakani kwa miaka 32.

Wakati wa uongozi wake, nchi DRC ilibadilishwa jina na kuwa Zaire, iliyokuwa chini ya chama kimoja.

Wakati wa uongozi wa Mobutu, Laurent-Desire Kabila alianza harakati za kumwondoa madarakani na aliunda kundi la waasi, alipata msaada wa nchi jirani na mwaka 1997, alifanikiwa kuingia madarakani baada ya kumwangusha Mobutu.

Alipoingia madarakani, aliibadilisha jina ya nchi hiyo kutoka zaire na kuita Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini mwaka 2001, aliuawa baada ya kupigwa risasi na mlinzi wake.

Kuuawa kwa Laurent Kabila, ndiko kulikomleta madarakani mtoto wake Joseph Kabila Kabange, ambaye ameongoza kwa miaka 17 na sasa baada ya Uchaguzi wa leo Jumapili, anaondoka madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.