Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-UCHUMI

Kumi na tisa wauawa katika maandamano yanayoendelea Sudan

Serikali ya Sudan inasema watu 19 wamepoteza maisha katika maandamano yanayoendelea katika miji mbalimbali nchini humo kulalamikia kupanda kwa bei ya mkate.

Waandamanaji katika mji wa Khartoum, Sudan, Desemba 25, 2018.
Waandamanaji katika mji wa Khartoum, Sudan, Desemba 25, 2018. REUTERS / Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Maandamano yaliyoanza kwa amani, yamegeuka na kuwa makabiliano makali kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama hasa jijini Khartoum.

Licha ya malalamiko ya kupanda kwa bei ya mkata, waandamanaji pia wanamtaka rais Omar Al Bashir ajiuzulu.

Wanahabari nchini humo wameungana na Madakatari kugoma, ili kuunga mkono maandamano haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.