Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-UCHAGUZI-SIASA

Wananchi wa Madagascar wapiga kura kumchagua rais wao mpya

Raia wa Madagascar wanapiga kura leo Jumatano ikiwa ni duru ya pili ya uchaguzi unaowakutanisha marais wawili wa zamani wa taifa hilo, Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina.

Mjadala wa televisheni kati ya wagombea urais wawili, Andrey Rajoelina na Marc Ravalomanana tarehe 9 Desemba 2018.
Mjadala wa televisheni kati ya wagombea urais wawili, Andrey Rajoelina na Marc Ravalomanana tarehe 9 Desemba 2018. Mamyrael / AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hawa wanaenda kwenye uchaguzi wa duru ya pili baada ya kuibuka wa kwanza na wapili katika uchaguzi wa duru ya kwanza mwezi Novemba.

Katika duru ya kwanza, Rajoelina alishinda kwa asilimia 39.23 huku mpinzani wake Ravalomanana, akimaliza wa pili kwa asilimia 35.55.

Zaidi ya wapiga kura milioni kumi wanashiriki uchaguzi huo kumchagua rais wao mpya.

Vituo vya kupigia kura 25,000 vimefunguliwa saa 12:00 asubuhi saa za Madagascar (sawa na saa 11:00 saa za Afrika ya Kati) na vinatarajiwa kufungwa saa 11:00 ( sawa na saa 10 Alaasiri saa za Afrika ya Kati) leo Jumatano.

Hata hivyo, kuna wasiwasi wa kutokea kwa machafuko iwapo mmoja wa wagombea atakataa kukubali matokeo baada ya zoezi la upigaji kura kumalizika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.