Pata taarifa kuu
SOMALIA-MAREKANI-SIASA-USALAMA

Afisa wa zamani wa Al Shabab atengwa katika siasa Somalia

Serikali ya Somalia, inasema msemaji wa zamani wa kundi la Al Shabab Mukhtar Robow ameondolewa katika orodha ya wale wanaowania uongozi wa majimbo nchini humo.

Serikali ya Mogadishu imemzuia Mukhtar Robow, mmoja wa waanzilishi wa Al Shabab, kuwania uongozi  katika Jimbo la Kusini Magharibi mwa Somalia. Hali hii ilisababisha tume ya uchaguzi katika eneo hiulo kujiuzulu.
Serikali ya Mogadishu imemzuia Mukhtar Robow, mmoja wa waanzilishi wa Al Shabab, kuwania uongozi katika Jimbo la Kusini Magharibi mwa Somalia. Hali hii ilisababisha tume ya uchaguzi katika eneo hiulo kujiuzulu. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili, kutakuwa na Uchaguzi wa majimbo na Robow aliyekamatwa wiki hii, alikuwa ametangaza kuwa angewania urais wa jimbo la Kusini Magharibi.

Wakati wa kukamatwa kwake katika eneo la Baidoa, watu wengine 11 walipoteza maisha.

Wakati huo huo Jeshi la Marekani limesema limewaua wapiganaji 62 wa kundi la kiislamu la Al Shabab kwa mashambulizi sita ya anga nchini Somalia.

Haya ni mashambulizi makubwa kuwahi kutokea tangu mwezi Novemba mwaka 2017, pale Marekani ilipowaua wanamgambo 100.

Kumekuwa na ongezeko la mashambulizi ya anga tangu Rais wa Marekani Donald Trump aingie madarakani mwezi Januari mwaka 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.