Pata taarifa kuu
TUNISIA-SAUDI ARABIA-USHIRIKIANO

Ziara ya Mwanamfalme wa Saudia nchini Tunisia yazua sintofahamu

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman, anatarajiwa Jumanne hii Novemba 27 kuzuru Tunisia kama sehemu ya ziara yake katika nchi kadhaa za Kiarabu. Mohamme bin Salman atapokelewa na Rais wa nchi hiyo.

Bango kubwa ambapo kumewekwa picha ya Mwanamfalme Mohammed bin Salman akishikilia msumeno, huku likiandikwa maneno kama haya "Ziara yako isije kuleta madhara kwa taifa la Tunisia".
Bango kubwa ambapo kumewekwa picha ya Mwanamfalme Mohammed bin Salman akishikilia msumeno, huku likiandikwa maneno kama haya "Ziara yako isije kuleta madhara kwa taifa la Tunisia". FETHI BELAID / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo vyama vya kiraia vinapinga ziara hiyo, vikimshtumu Mwanamfalme Mohammed bin Salman kuhusika katika mauji ya kikatili ya mwandishi wa nchi hiyo Jamal Khashoggi, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa babake.

Khashoggi aliauwa alipokuwa amekwenda katika Ubalozi wa nchi yake jijini Istabul nchini Uturuki, tarehe mbili mwezi Oktoba.

Saudi Arabia inasaidia kifedha nchi kadhaa za Kiarabu, lakini Mwanamfalme kutoka nchi hiyo anapingwa vikali kuzuru nchi hizo.

Kwa upande wa Messaoud Romdhani, kiongozi wa shirika linalojihusisha na masuala ya uchumi na kijamii (FTDES), anasema kupingwa kwa ziara hiyo kunaendana na sababu tatu kubwa: "kwanza ni mauaji ya Khashoggi, kitendo cha kikatili. Pili, ni vita vya Yemeni ambapo maelfu ya raia, wanauawa na wengine kujeruhiwa. Na tatu, hali ya haki za binadamu nchini Saudi Arabia. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.