Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-SIASA-UCHUMI

Upinzani kuandamana Septemba 29 kupinga hali ya kiuchumi Burkina Faso

Upinzani nchini Burkina Faso umetoa wito kwa wafuasi wake kuandamana tarehe 29 Septemba kupinga utawala wa Roch Marc Christian Kaboré, ukisema kuwa umesababisha "hali ya uchumi kuwa mbaya", tangu rais huyo kuingia madarakani mwezi Novemba 2015.

Kiongozi wa upinzani Burkina Faso Zéphyrin Diabré, akikaribishwa na wafuasi wake Ouagadougou, Aprili 29, 2017.
Kiongozi wa upinzani Burkina Faso Zéphyrin Diabré, akikaribishwa na wafuasi wake Ouagadougou, Aprili 29, 2017. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo ambayo yatafanyika nchini kote, yatakua ya kwanza ya aina yake kuandaliwa na upinzani tangu uchaguzi wa Rais Kaboré.

Upinzani unaomba wananchi wote wa Burkina Faso kuitikia maandamano hayo kupinga utawala wa Rais Kaboré, ambao unaonekana kama utawala wa chama kimoja na washirika wake pekee bila upinzani.

Maandamano hayo ya amani yatafanyika Jumamosi, Septemba 29, 2018 katika mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou, na maeneo mbalimbali ya nchi," amesema kiongozi wa upinzani Zéphyrin Diabré ambatana na wanasiasa wengine wa upinzani, katika taarifa kwa vyombo vya habari.

"Ni hatua dhidi ya utawala unaosababisha machafuko katika nchi yetu. Tumetolea wito wananchi wote wa Burkina Faso, ikiwa ni pamoja na makundi mbalimbali, vyama vya siasa, mashirika ya kiraia na vyama vya wafanyakazi amesema Diabré.

Tangu kuingia madarakani mnamo Novemba 2015, Rais Kaboré na serikali yake wameendelea kukosolewa na upinzani, ikiwa ni pamoja na kambi yake mwenyewe.

"Kama upinzani umeafikiana tarehe hiyo, ni kwa sababu wametaka kutoa nafasi kwa utawala kujirekebisha na kuchukua mwelekeo sahihi," ameongeza Zéphyrin Diabré, pia kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha UPC.

Alipochaguliwa mnamo mwezi Novemba 2015, Rais Kaboré aliahidi kupunguza umasikini lakini bado hajapata euro bilioni 28 ili kufadhili Mpango wa Taifa wa Uchumi na Maendeleo ya Jamii (PNDES) ulioandaliwa ktekelezwa kwa muhula wake ambao utamalizika mwaka 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.