Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-SIASA

Jean-Pierre Bemba atengwa katika uchaguzi wa urais DRC

Mahakama ya Katiba nchini DRC imetoa uamuzi wake baada ya Jean-Pierre Bemba na wanasiasa wengine watano kukata rufaa kufuatia uamuzi wa Tume huru ya Uchaguzi nchini humo (CENI) kuwazuia kuwania katika ucahaguzi wa urais wa Desemba 23.

Hatua ya kwanza ya Jean-Pierre Bemba nchini DRC baada ya miaka 11 kutokuwepo, Agosti 1, 2018 (picha ya kumbukumbu)
Hatua ya kwanza ya Jean-Pierre Bemba nchini DRC baada ya miaka 11 kutokuwepo, Agosti 1, 2018 (picha ya kumbukumbu) © RFI/Florence Morice
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Katiba imethibitisha uamuzi wa CENI na kusema kuwa Jean-Pierre Bemba hana sifa ya kuwania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23 kufuatia hukumu aliyopewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa kosa la kuhonga mashahidi. Kati ya wagombea sita waliozuiwa na Tume ya Uchaguzi kuwania katika uchaguzi wa urais nchini DRC, wawili wamerudishiwa haki ya kuwania.

Miezi mitatu iliyopita, hakuna mtu aliyefikiria kuwa Jean-Pierre Bemba atakuwa katika kinyang'anyiro cha urais. Lakini kutokana na tangazo la kuachiliwa kwake huru, kiongozi huyo wa zamani wa waasi alikua na matumaini ya kuwania katika uchaguzi wa urais. Alikua hajarudi DRC kwa zaidi ya miaka 10.

Jean-Pierre Bemba anatajwa kama mpinzani mkuu anayesumbua utawala wa Joseph Kabila na chama chake cha PPRD katika uchaguzi ujao.

Hivi karibuni Bemba aliachiliwa katika kesi dhidi ya uhalifu wa kivita na mahakama baada ya kutumikia kifungo cha miaka kumi jela.

Mwezi uliopita alirejea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kupokelewa kwa mapokezi makubwa kutoka kwa wafuasi wake.

“Ikiwa hatuna mkakati wa pamoja, haiwezekani kuokoa Congo. Tuko mbele ya watu ambao hawaheshimu sheria, “ amesema Eve Bazaiba, katibu mkuu wa chama cha MLC cha Jean-Pierre Bemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.