Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-EMMERSON MNANGAGWA-SIASA-UCHAGUZI

Mnangagwa aapishwa, aahidi kulinda haki za raia wa Zimbabwe

Emmerson Mnangagwa ameapishwa kushika hatamu za uongozi wa Zimbabwe kwa miaka mitano ijayo, karibu mwezi mmoja baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson mnangagwa ameapishwa leo kuliongoza taifa hilo kwa miaka mitano
Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson mnangagwa ameapishwa leo kuliongoza taifa hilo kwa miaka mitano AFP
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya katiba Ijumaa wiki hii ilithibitisha ushindi wa asilimia 50 aliopata Mnangagwa katika uchaguzi wa Julai 30, ikitupilia mbali shauri lililofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa upinzani Nelson Chamisa.

Mamia kwa maelfu ya watu walimiminika katika Uwanja wa Taifa Mjini Harare, kushuhudia kuapishwa kwa Mnangagwa ambaye alichukua madaraka Novemba mwaka jana, baada ya Jeshi kuingilia kati na kumuondoa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe.

"Mimi Emmerson Dambudzo Mnangagwa naapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Zimbabwe, na nitaiheshimu, kuitetea na kuilinda katiba ya Zimbabwe,"alisema kiongozi huyo katika kiapo kilichoongozwa na Jaji Mkuu Luke Malaba.

Kiongozi huyo ameahidi kulinda na kutetea haki za raia wa Zimbabwe.

Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali  wa Afrika akiwemo, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa na rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Hata hivyo Mnangagwa anakabiliwa na kazi nzito ya kurejesha umoja katika taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.