Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Mahakama ya Katiba yamtangaza Ibrahim Boubacar Keita mshindi wa uchaguzi Mali

Rais wa Mali anayemaliza muda wake Ibrahim Boubacar Keïta ametangazwa rasmi mshindi wa uchaguzi wa urais na anatarajia kutawazwa na kuanza muhula wake wa pili wa miaka mitano tarehe 4 Septemba, Mahakama ya Katiba imetangaza.

Rais mteule Ibrahim Boubacar Keita.
Rais mteule Ibrahim Boubacar Keita. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Ninamtangaza Ibrahim Boubacar Keïta kuwa ni mshindi wa uchaguzi wa urais wa Agosti 12" , amesema Mkuu wa mahakama, Manassa Danioko baada ya kuskilizwa kwa muda wa saa moja kesi ya madai ya wizi wa kura iliyowasilishwa na kiongozi wa upinzani, Soumaïla Cissé.

Lakini Cisse, ambaye katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2013 alikubali haraka kuwa alishindwa, katika uchaguzi huu wa Agosti 12 alifutilia mbali matokeo ya uchaguzi, akitaja kuwa uchaguzi huo "uligubikwa na wizi wa kura". Kulingana na mahesabu yake mwenyewe, "alishinda uchaguzi huo kwa 51.75% ya kura".

Bw Keita, mwenye umri wa miaka 73, alipata 67.16% ya kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa Agosti 12, dhidi ya mpinzani wake Soumaila Cisse, waziri wa zamani wa fedha, mwenye umri wa miaka 68, ambaye alipata 32.84%, amesema Bi Danioko.

Mahakama imefutilia mbali madai yasiyo kuwa na msingi na yasiyokubalika na ambayo hayana ushahidi yaliyowasilishwa na kiongozi wa upinzani, ambaye alitoa wito kwa maelfu ya wafuasi wake walioandamana siku ya Jumamosi huko Bamako "kuendelea kupambana".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.