Pata taarifa kuu
GUINEA BISSAU-USALAMA

Askari kumi wazuiliwa kwa shutma za kutaka kumuua mkuu wa majeshi Bissau

Askari kumi wa Guinea-Bissau wanazuiliwa baada ya kushtumiwa kwamba walitaka kumuua mkuu wa majeshi ya nchi hiyo mnamo mwezi Desemba 2017. Askari hao wanazuliwa katika "mazingira mabaya" na "hakuna ushahidi wowote" dhidi yao, mwanasheria wao amesema.

Rais mteule José Mario Vaz, upande wa kulia, na mkuu wa majeshi ya Guinea-Bissau, Jenerali Antonio Indjai, katikati, baada ya mkutano katika ikulu huko Bissau Mei 20, 2014.
Rais mteule José Mario Vaz, upande wa kulia, na mkuu wa majeshi ya Guinea-Bissau, Jenerali Antonio Indjai, katikati, baada ya mkutano katika ikulu huko Bissau Mei 20, 2014. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Askari hao kumi, wengi wao wakiwa maafisa wa ngazi ya juu katika makao makuu ya jeshi huko Bissau, walikamatwa mapema mwezi Desemba 2017. Walituhumiwa kutaka kumuua Mkuu wa majeshi, Jenerali Biague Na Ntam Wakili Ricardo Nancassa ameliambia shirika la habari la AFP.

Walikuwa wanasubiri kurudi mjini Bissau kwa Jenerali Ntam, ambaye alikuwa nje ya nchi kwa sababu za matibabu, ili kutekeleza mpango wao kwa mujibu wa upande wa mashitaka, Wakili Nancassa amesema.

Tangu wakamatwe, "hawajafikishwa mbele ya mahakama ili wasikilizwe kuhusu tuhuma dhidi yao. Huu ni ukiukaji wa wazi wa sheria na uhuru kwa wafungwa. Wao wanazuiliwa kinyume cha sheria," wakili Nancassa amestumu.

"Hii ni kinyume na sheria ya nchi yetu, hadi sasa hakuna ushahidi wowote ambao umewasilishwa dhidi yao," amesema.

"Watu hawa bado wanazuiliwa katika mazingira mabaya katika jela la kambi ya jeshi la anga bila hata hivyo kuepo na ushahidi tosha kuhusu shutma inayowakabili, " Nancassa ameongeza, huku akiomba wateja wake waachiliwe huru mara moja.

Mahakama ya kijeshi haijasema chochote kuhusiana na kesi hiyo, kwa mujibu wa shiika la habari la AFP.

Guinea-Bissau, koloni ya zamani ya Ureno, imekuwa miaka katika mgogoro wa kisiasa na kijeshi ambapo mara nyingi jeshi limehusishwa.

Nchi hii iliingia katika mgogoro wa kisiasa tangu rais Jose Mario Vaz kutimuliwa mnamo mwezi Agost 2015 na Waziri Mkuu wake, Domingos Simões Pereira, mkuu wa chama cha PAIGC, pia chama cha Bw Vaz.

Makubaliano mapya ya kuondokana na mgogoro huo yalifikiwa katika mkutano wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) Aprili 14 mjini Lome.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.