Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Upinzani wajaribu kumteua mgombea mmoja katika uchaguzi DRC

Upinzani nchini DRC umetoa wito kwa vyama vyote vya upinzani kuungana n akumteua mgombea mmoja pekee atakaye pambana na mgombea wa chama tawala na washirika wake katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23.

Felix Tshisekedi na wawakilishi wengine wa upinzani watoa wito kwa vyama vingine vya upinzani kuteua mgombea mmoja katika uchaguzi wa Desemba 23.
Felix Tshisekedi na wawakilishi wengine wa upinzani watoa wito kwa vyama vingine vya upinzani kuteua mgombea mmoja katika uchaguzi wa Desemba 23. JUNIOR D. KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Upinzani pia unataka serikali kufuta hatua zake dhidi ya Moise Katumbi na kumuachia aweze kurudi nyumbani. Kiongozi wa chama cha UDPS Felix Tshisekedi, Vital Kamerhe kiongozi wa chama chaUNC na kiongozi wa Congo na Biso Freddy Matungulu, walikuepo katika sherehe ya kutafuta mgombea wa upinzani Jumatatu wiki hii.

Jean-Pierre Bemba Gombo kiongozi wa chama cha MLC na Gavana wa zamani wa mkoa wa Katanga Moise Katumbi Chapwe waliwakilishwa katika sherehe hiyo. Hata hivyo chama cha ECiDé kinachoongozwa na Martin Fayulu hakikuepo katika sherehe hiyo.

Wagombea sita waliotia saini kwenye tamko la pamoja la upinzani wamekaribisha msimamo wa Joseph Kabila, ambaye hatimaye alikubali kuheshimu katiba, kwa kutowania muhula wa tatu katika uchaguzi wa Desemba 23. Upinzani, umesema huo ni ushindi wa kihistoria kwa wananchi wa DRC.

Hayo yanajiri wakati ambapo Tume ya Uchaguzi CENI imefahamisha kupokea na kusajili majina ya watu 25 ambao watagombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Disemba 23. Miongoni mwa wagombea hao yumo mwanamke mmoja.

Wagombea wa kiti cha urais walisajliwa kuanzia Julai 25 na kumalizika Agosti 8.

Miongoni mwa wagombea yumo pia msemaji wa mwisho wa rais wa zamani Mobutu, Tryphon Kin-Kiey Mulumba ambe pia alikuwa mstari wa kwanza kumtetea rais Kabila kusalia madarakani na muhula wake wa tatu.

Jean-Pierre Bemba, Félix , Vital Kamerhe ndio wagombea wakubwa, wapinzani wa chama tawala na uongozi wa rais Joseph Kabila.

José-Marie Ifoku ndio mgombea pekee mwanamke aliejiandiakisha kugombea kiti cha urais katika uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.