Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-UNHCR-USALAMA

UNHCR yaendelea na jitihada za kusaidia wakimbizi wa ndani Ethiopia

Shirika la Umoja wa Mataifa (UNHCR) linaendeleza jitihada zake za kusaidia takribani watu milioni moja ambao wamejikuta ni wakimbizi wa ndani nchini Ethiopia kufuatia ghasia za hivi karibuni kusini-magharibi mwa nchi hiyo.

Maandamano ya watu kutoka jamii ya watu wachache ya Oromo nchini Ethiopia, Oktoba 2, 2016.
Maandamano ya watu kutoka jamii ya watu wachache ya Oromo nchini Ethiopia, Oktoba 2, 2016. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Hali si shwari ikielezwa kuwa baadhi ya watu wanalala nje, wajawazito hawana huduma, huku wakimbizi hao wakielezea mateso yanayowakumba kama vile ubakaji, mauaji, nyumba zao kuchomwa moto sambamba na mifugo yao.

UNHCR inasema ghasia hizo ambazo ni pamoja na mapigano ya kikabila kwenye maeneo ya mpakani ya jamii ya kusini na mkoa wa Oromia yameibuka wakati tayari kunaripotiwa ukame uliosababisha mvutano baina ya wakazi wa maeneo hayo.

Msemaji wa UNHCR mjini Geneva, Uswisi, Andrej Mahecic akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa wiki hii amesema wakimbizi hao wa ndani hivi sasa wanahitaji huduma za dharura ikiwa ni pamoja na malazi na kuendeleza juhudi za mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa.

“Tayari UNHCR imesambaza vikasha 50,000 vyenye huduma muhimu ikiwemo vyombo vya kupikia, mikeka ya kulalia, mablanketi na makaratasi ya nailoni yanayofaa kutengenezea makazi, “ amesema Bw Mahecic.

Serikali ya Ethiopia na wadau wake wa kibinadamu wametangaza ombi la pamoja la zaidi ya dola milioni 117 ili kukabiliana na suala linalotatiza zoezi la utoaji wa huduma kwa wakimbizi hao wa ndani.

Msemaji wa UNHCR amesema serikali ya Ethiopia imeahidi kuendeleza juhudi za maridhiano kwenye eneo hilo ili kuleta maelewano baina ya pande husika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.