Pata taarifa kuu
CAR-URUSI-USALAMA

Uchunguzi kuhusu mauaji ya wanahabari watatu waanzishwa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mauaji ya waandishi wa habari watatu wa Urusi ambao walikuja nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuchunguza kuwepo kwa kitengo cha askari mamluki wa Wagner, yamegonga vichwa vya habari nchini humo.

Askari wa Ufaransa wakikosi cha Sangaris, wakipiga doria katika mitaa ya Sibut, kaskazini mwa Bangui, Septemba 25, 2015. (Picha ya kumbukumbu).
Askari wa Ufaransa wakikosi cha Sangaris, wakipiga doria katika mitaa ya Sibut, kaskazini mwa Bangui, Septemba 25, 2015. (Picha ya kumbukumbu). EDOUARD DROPSY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imeanzisha uchunguzi ili kujua sababu za mauaji ya waandishi hao wa habari. Uchunguzi huo unasimamiwa na Wizara ya Sheria, kupitia Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Bangui. Uchunguzi huu unaendeshwa na polisiya Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa msaada wa polisi wa Umoja wa Mataifa.

Timu ya UNPOL ilizuru Sibut mapema Jumatano asubuhi, Agosti 1, ili kusaidia timu ya polisi inayochunguza kisa hiocho kwenye eneo la tukio.

Urusi haishiriki moja kwa moja katika uchunguzi huo.

Kikosi hiki cha askari mamluki kinadhaminiwa na ikulu ya Kremlin kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya usalama kutoka Urusi.

Tayari mauaji ya waandishi hao wa habari yameibua suala la kuzorota kwa usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mauaji haya yanahusiana na kutolewa kwa ripoti ya jopo la wataalam wa Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa hati hii, Urusi kupeleka kikosi hiki nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, baada ya kuombwa na serikali ya Touadéra- kumezua hali tofauti na ilivyotarajiwa na kusababisha nchi hii kukumbwa na machafuko mapya.

Hali hii ilianza mnamo mwezi Desemba mwaka jana wakati Urusi iliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuta vikwazo vya silaha dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ilielewka kuwa, Urusi inataka kusaidia majeshi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kujiimarisha dhidi ya makundi ya waasi yanayodhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo. Wanadiplomasia walikuwa wamepinga ombi hilo la Urusi kwa muda mrefu, wakiwa na wasiwasi kwamba silaha hizo huenda zingeenezwa katika nchi hiyo ambayo inaendelea kukumbwa na machafuko, lakini baadaye waliachia ngazi na kukubali ombi hilo la Urusi.

Karibu miezi mitano baadaye, mtazamo wa wataalamu wa Umoja wa Mataifa umeeleweka: serikali kupewa silaha imefufua mashindano ya kununua silaha kati ya makundi ya waasi na hasa baadhi ya makundi yaliyogawanyika kutoka kundi la waasi la Seleka. Makundi haya yananunua silaha kutoka nchi jirani ya Sudan, ambayo inauza silaha zake katika sehemu ya mchakato wa kuwapokonya silaha raia wanaozimiliki kinyume cha sheria huko Darfur.

Makundi haya yaliambia wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuwa yana wasiwasi kwamba serikali ya Touadera inaandaa vita dhidi yao. Chaguo la kijeshi, lililopendekezwa na serikali ya Bangui badala ya chaguo la kisiasa, limewafanya wao kujiimarisha tena kijeshi, kwa mujibu wa vyanzo kutoka makundi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.