Pata taarifa kuu
DRC-KABILA-SIASA-USALAMA

Hotuba ya rais Kabila yaacha wengi vinywa wazi

Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila katika hotuba yake kwa wabunge amesema ataheshimu katiba ya nchi hiyo bila hata hivyo kueleza iwapo atawania tena urais, suala ambalo raia wa DRC walikuwa wanasubiri kusikia.

Joseph Kabila, Julai 19, 2018.
Joseph Kabila, Julai 19, 2018. © Junior D. KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kabila kwa utani alisema anafahamu kile ambacho wengi walipenda kusikia akitamka kama alivyofanya rais wa zamani wa nchi hiyo Joseph Desire Mobutu wakati akitangaza mfumo wa vyama vingi.

Muda mwingi wa hotuba yake alielezea mafanikio ya uongozi wake tangu mwaka 2001 na kusisitiza kuwa nchi yake haiko tayari kupokea mafunzo yoyote kutoka kwa wahalifu wa demokrasia.

Hotuba hiyo imepokewa kwa mitazamo tofauti na wanasiasa nchini humo baadhi wakimsifu huku wengine wakisikitishwa kuona hajaweka wazi nia yake ya kuwania uchaguzi au la.

Kamati ya walei wa Kanisa Katoliki kupitia msemaji wake, Jonas Chombela, imesema hakuna jipya katika hotuba hiyo.

Upande wake mwenyeti wa shirika linalowania demokrasia na utawala bora nchini DRCongo CEPADO Omar Kavota amesema Rais Joseph Kbila amewaacha watu na kiu hasa katika kufahamu iwapo atawania uchaguzi au la.

Hotuba hiyo ya rais Kabila imekuja ikiwa ni miezi mitano tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi nchini DRCongo, huku katiba ikiwa haimruhusu Rais Kabila kuwania uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.