Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-MANDELA-UHURU

Graça Machel awataka vijana wa Afrika kuwa na mtazamo wa Mandela

Afrika Kusini inaadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Nelson Mandela huko Johannesburg Jumanne, Julai 17. Kila mwaka, hotuba hutolewa na kiongozi maarufu kimataifa.

Nelson Mandela na mkewe Graça Machel, Cape Town, Februari 11, 2010.
Nelson Mandela na mkewe Graça Machel, Cape Town, Februari 11, 2010. Reuters / S. van Zuydam
Matangazo ya kibiashara

Kwa mwaka huu, itakuwa zamu ya Barack Obama, ambaye tayari ameliwasili nchini Afrika Kusini anakotarajiwa kutoa hotuba ya kusherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwa aliyekuwa rais wa kwanza mweusi Nelson Mandele aliyefariki dunia mwaka 2013.

Shirika la Rais wa zamani wa Marekani sasa linafanya mkutano wa wiki moja nchini Afrika Kusini unaojumuisha viongozi vijana wa Kiafrika. Vijana 200 ndio wanashiriki mkutano huo, kutoka nchi 44 za bara hilo, katika hali ya kubadilishana na kujifunza kuwa viongozi wa kesho.

Mwansa Lubeya kutoka Zambia, ambaye ni mtu maarufu kati ya vijana 200 maarufu barani Afrika ni miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo. Bi Lubeya, alijulikana sana kwa kampeni zake za kuzuia kansa.

"Warithi wa Mandela wako hapa hapa hapa leo. Na nadhani Mandela alionekana na kujitolea kati ya viongozi wengine wote kwa uadilifu wake. Alijua mipaka yake. Alikuwa aakitia mbele ubinadamu, "Bi Lubeya amesema.

Mjane wa Mandela, Graça Machel amesema dunia bado ipo mbali sana kufikia malengo aliyokuwa nayo Mandela kuhakikisha kuwa, watu wanakuwa huru kabisa.

Aidha, ametoa wito kwa watu duniani, kutumia maadhimisho hayo, kupambana na ubaguzi lakini pia kuinua kiwango cha elimu.

Viongozi wapya wamekusanyika ili kuendelea na mapambano ya Mandela, amesema mjane wa Mandela, Graça Machel.

"Mabadiliko makubwa ya bara huhusisha mtandao mkubwa wa viongozi wadogo ambao, pamoja, wanaweza kuleta nguvu kwa kubadili," ameongeza Graça Machel.

Madhimisho haya yamekuja, siku moja kabla ya siku za kuazaliwa kwa Mandela ambayo ni kesho tarehe 18.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.