Pata taarifa kuu
DRC-BEMBA-SIASA-USALAMA

Jean-Pierre Bemba atangazwa mgombea urais na chama chake

Chama cha upinzani cha MLC kimemtangaza rasmi kiongozi wa chama hicho, Jean-Pierre Bemba, kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi wa Desemba 23 mwaka huu nchini humo.

Wafuasi wa Jean-Pierre Bemba wakifurika mitaani mjini Kinshasa baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, kufuta hukumuiliyokua ikimkabili kiongozi wao, Juni 8, 2018.
Wafuasi wa Jean-Pierre Bemba wakifurika mitaani mjini Kinshasa baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, kufuta hukumuiliyokua ikimkabili kiongozi wao, Juni 8, 2018. JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imechukuliwa baaada ya Bw Bemba kuachiliwa huru na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, siku kadhaa zilizopita, baada ya kushikiliwa na mahakama hiyo kwa zaidi ya miaka 3 kwa shutma za uhalifu dhidi ya binadamu, baada ya kuhusishwa katika mauaji yaliyotekelezwa na wapiganaji wake nchini Afrika Kusini.

Tangazo hilo lilitolewa wakati chama hicho kilipokua kikifungua mkutano wake Alhamisi wiki hii jijini Kinshasa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, katibu mkuu wa chama hicho Eve Bazaiba amevitaka vyama vya upinzani kuungana pamoja katika kuhakikisha vinashinda kwenye uchaguzi huo.

Mbali na maelfu ya wafuasi wa chama hicho waliohudhuria mkutano huo mkubwa ni pamoja na Felix Tshisekedi wa chama cha Upinzani cha UDPS, Emmanuel Shadary wa chama tawala cha PPRD pia Vital Kamerhe wa chama cha UNC, Miongoni mwa wengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.