Pata taarifa kuu
MALAWI-SIASA-USALAMA

Maalbino sita kuwania katika Uchaguzi mkuu nchini Malawi

Maalbinos sita wamepanga kushiriki katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwaka ujao nchini Malawi. Wagombea wote sita ni wanachama wa Chama cha wenye ulemavu wa ngozi, Albino, (APAM).

Malbinos huko Dar es Salaam (Tanzania) kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi (maalbino) mnamo mwaka 2016.
Malbinos huko Dar es Salaam (Tanzania) kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi (maalbino) mnamo mwaka 2016. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Maalbino hao wanalenga kulinda maslahi ya jamii yao, ambayo mara nyingi inaathiriwa na unyanyasaji na chuki.

Kwa mujibu wa Overstone Kondowe, mkurugenzi wa APAM, kuwa nafasi katika bunge au katika moja ya halmashauri ya wilaya nchini itawawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi yao.

Katika baadhi ya nchi za Afrika, maalbino mara nyingi huuawa na viungo vyao hutumiwa kwa imani za kishirikiana kama vinaleta utajiri na bahati.

Mwaka 2014, kwa mujibu wa APAM, maalbino 22 waliuawa nchini Malawi kwa jumla ya kesi 148 za ukatili zilizoorodheshwa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.