Pata taarifa kuu
DRC-ICC-BEMBA-HAKI

ICC yamwachilia huru kwa masharti Jean Pierre Bemba

Majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC wameagiza kuachiwa huru kwa masharti kwa aliyekuwa makamu wa rais wa zamani wa DRC, Jean-Pierre Bemba ambaye juma lililopita alifutiwa mashtaka ya makosa ya kivita na dhulma dhidi ya binadamu.

Wafuasi wa Jean-Pierre Bemba wakisherehekea kuachiliwa huru kwa kiongozi wao kwenye makao makuu ya chama chake cha MLC, uamuzi uliochukuliwa na mahakama ya ICC Juni 8 katika.
Wafuasi wa Jean-Pierre Bemba wakisherehekea kuachiliwa huru kwa kiongozi wao kwenye makao makuu ya chama chake cha MLC, uamuzi uliochukuliwa na mahakama ya ICC Juni 8 katika. JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Bemba mwanasiasa maarufu nchini mwake na mpinzani mkubwa wa rais Joseph Kabila ameachiwa baada ya kushinda rufaa aliyokata kwenye mahakama hiyo kupinga adhabu ya kifungo cha miaka 18 jela baada ya kukamatwa nchini Ubelgiji mwaka 2016.

Bemba alipatikana na hatia mwezi Machi mwaka 2016 kwa makosa ya uhalifu, uliotokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003 na akahukumiwa 21 Juni.

Mahakama hiyo imetoa uamuzi huo kufuatia rufaa aliyoiwasilisha kupinga hukumu hiyo.

Uamuzi wa mahakama umepokelewa kwa shangwe na wafuasi wake waliokuwepo ukumbi wa mahakama. Mjini Kinshasa, wafuasi wake wameendelea kusheherekea tukio hilo wakisema kiongozi wao ametendewa haki.

Hata hivyo majaji wa mahakama hiyo wamemuachia kwa masharti ya kutozungumza na vyombo vya habari wala kuwasiliana na mashahidi katika kesi yake, akisubiri hukumu kuhusu tuhuma za kuhonga mashahidi na kutoa ushahidi wa uongo mahakamani.

Ikiwa Bemba ataachiwa huru anatajwa kuwa kinara katika siasa za nchi hiyo na tayari chama chake cha MLC kinamtaja kama mgombea wao katika uchaguzi wa Desemba 23 mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.